Mpeni Kaisari

Mpeni Kaisari
ChoirChrist The King Bungoma
AlbumPilka Pilka
CategoryOffertory/Sadaka
ComposerOchieng Odongo

Mpeni Kaisari Lyrics

1. Vipaji tumepewa, mapato tumepata
Lakini binadamu tunashindwa kushukuru
Wakati tunaomba, tunajinyenyekesha
Lakini tukipata mikono yetu birika


Mpeni kaisari, yaliyo yake
Mpeni Mungu (yale) yaliyo yake Mungu *2


2. Mifugo tunafuga, nafaka tunavuna
Lakini kila siku tunakula na kusaza
Kumbuka kuna wale, wasio na chochote
Hawawezi kupata, hata kikombe cha chai

3. Tunapofanya kazi, twapata mishahara
Shughuli zetu sisi kuingia kwenye baa
Ikiwa zitabaki, twakuja kanisani
Twamtolea Mungu, shilingi moja na tano

4. Tukiwa na wagonjwa hatuwasaidii
Wakati wamekufa tunachanga kwa huzuni
Twachukua mikopo, kwa mambo ya anasa
Ujenzi wa kanisa, twalazimishwa kutoa.

5. Kumbuka Ibrahimu, alitoa mwanawe
Kama sadaka kwake Mungu Baba wa mbinguni
Na sisi kwa furaha, tupeleke zawadi
Itakayopendeza, kama ile ya Abeli

Favorite Catholic Skiza Tunes

SMS the Skiza ID to 811 to get the song as your Skiza tune.

TitleSKIZA ID
Cha Kutumaini Sina 5814855
Roho Yangu na Ikuimbie 5814859
Nikupe Nini Mungu Wangu 7482438
Sasa Wakati Umefika 7482439
Bwana Kama Wewe Ungehesabu Maovu Yetu 7482444
Nitakwenda Mimi Mwenyewe 7482440
Zaeni Matunda Mema 5814860
Huniongoza Mwokozi 5814856
Utukuzwe Ewe Baba 7482441
Tazama Tazama 7482442