Mwili Wako

Mwili Wako
ChoirTBA
CategoryEkaristia (Eucharist)
ComposerF. A. Nyundo

Mwili Wako Lyrics

Mwili wako na damu yako imetushibisha
Karamu uliyoandaa imetushibisha

 1. Mwili wako tunaokula ni chakula kweli
  Damu yako tunayokunywa ni kinywaji safi
 2. Tukipokea kwa imani tutaokoka tu
  Karibu Yes undani yetu ukae daima
 3. Kaa nasi Ee Yesu mwema utupe uzima
  Utupe nguvu Rohoni mwetu milele milele
 4. Mwili wako na damu yako vyatushirikisha
  Uzidi pia kutualika kwenye meza yako
 5. Upendo wako Yesu mwema, utuzidishie
  Utuongoze maishani na tukufikie