Login | Register

Sauti za Kuimba

Acheni Visingizio Lyrics

ACHENI VISINGIZIO

@ Deo Kidaha

Acheni visingizio wanadamu,
acheni visingizio kwamba hali ni ngumu * 2
Nendeni mkatoe (vipaji) nendeni mkatoe vipaji
nendeni mkatoe vipaji kwa Bwana * 2

 1. Siyo ninyi wenye magari ya kifahari mnaodai hali ni ngumu.
  Siyo ninyi wenye fedha nyingi mifukoni mnaodai hali ni ngumu.
 2. Siyo ninyi wenye majumba ya kifahari mnaodai hali ni ngumu.
  Ndani yake mmejaza vito vya thamani mnaodai hali ni ngumu.
 3. Siyo ninyi mnaovuna mazao mengi mnaodai hali ni ngumu.
  Siyo ninyi mnaopokea mishahara mnaodai hali ni ngumu.
 4. Msidhani mmepata kwa uwezo wenu mnaodai hali ni ngumu.
  Bali ni Mungu aliye wajalia hayo mnaodai hali ni ngumu.
 5. Kumbukeni mjane alotoa dinari mnaodai hali ni ngumu.
  Hakubakiza chochote mfukoni mwake mnaodai hali ni ngumu.
Acheni Visingizio
COMPOSERDeo Kidaha
CATEGORYOffertory/Sadaka
MUSIC KEYD Major
TIME SIGNATURE2
4
SOURCEKirungu Kasulu
NOTES Open PDF
 • Comments