Sikuifukia Talanta Yangu

Sikuifukia Talanta Yangu
Performed by-
CategoryOffertory/Sadaka
ComposerVictor Aloyce Murishiwa
Views5,685

Sikuifukia Talanta Yangu Lyrics

  1. Sikuifukia talanta yangu, tazama Bwana naleta kwako leo
    Ninaleta shukrani zangu pokea Baba, ni mali yako

    Hivi vyote ni vyako, (mimi) nimepata kwa wema wako
    nasema asante Baba, asante, asante, asante * 2

  2. Umenijalia nguvu na akili, nikazitenda kazi
    Nimepata riziki zangu asante Baba asante
  3. Umenijalia siku za furaha nami nikafurahi
    Nikasifu jina la Bwana asante Baba asante
  4. Umemtoa mwanao Yesu Kristu aje kunikomboa
    Katika utumwa wa dhambi, asante Baba asante