Napiga Goti Langu

Napiga Goti Langu
ChoirTBA
AlbumRaha ya Ajabu
CategoryEkaristia (Eucharist)

Napiga Goti Langu Lyrics

Napiga goti langu (Bwana), nainamisha kichwa (chini)
{Kukuomba ewe Mungu-, unifungue moyo-
Nipate kushiriki- karamu takatifu-
Ili roho yangu dhaifu ipate wokovu} * 2

 1. Furaha ya moyo wangu ni wewe Bwana
  Matumaini ya moyo wangu ni kwako
  Ninajongea sasa kushiriki karamu takatifu, Bwana, wangu
 2. Ninaitikia mwaliko wako Bwana
  Moyo wangu unatetemeka kwa hofu
  Mwaliko wako umejaa upendo kwangu moyoni
 3. Kila tuulapo mwili wa Bwana Yesu
  Na kuinywa damu tunapata uzima
  Tumekombolewa kwa damu yake Mwanakondoo, Mwana wake Mungu