Ninakuabudu Mungu Wangu

Ninakuabudu Mungu Wangu
ChoirSt. Joseph Cathedral Dar-es-Salaam
CategoryEkaristia (Eucharist)
ComposerJoseph Makoye
Musical Notes
Time Signature3
4
Music KeyG Major
NotesOpen PDF

Ninakuabudu Mungu Wangu Lyrics

 1. Ninakuabudu Mungu wangu,
  Unayejificha altareni,
  Ninakutolea moyo wangu,
  Usiofahamu siri yako.
 2. Mafahamu yangu yadanganya,
  Yanapokuona na kugusa,
  Namsadiki Yesu hadanganyi,
  Yeye Mungu Mwana na ukweli
 3. Waficha Umungu msalabani,
  Na ubinadamu altareni,
  Nami naungama zote mbili,
  Kama mwivi yule mwenye toba.
 4. Thomas aligusa majeraha,
  Nami nasadiki bila shaka
  Ewe Yesu nipe pendo lako,
  Tumaini kwako na imani
 5. Umeteswa nini Bwana mwema,
  Kwa kunipa mkate wa uzima
  Yesu unifiche ndani yako,
  Ili nilionje pendo lako
 6. Yesu Pelikane nitazame,
  Na kwa damu yako nitakase
  Tone moja ndilo linatosha,
  Na dunia yote yaokoka
 7. Ndani ya mafumbo Yesu yumo,
  Atafunguliwa kwangu lini?
  Nikuone Yesu uso wako,
  Nishiriki nawe heri yako. Amina.