Ukaristia ni Yesu Lyrics

UKARISTIA NI YESU

 1. Ukaristia ni Yesu sadaka,
  Ukaristia ni Yesu chakula,
  Ukaristia ni mwili wa Yesu.
 2. Ukaristia ni mkate wa Mungu,
  Ukaristia ni mana ya kweli,
  Ukaristia ni uzima wetu.
 3. Ukaristia ni damu ya Yesu,
  Ukaristia ni kinywaji chetu.
  Ukaristia ni chem chem ya neema.
 4. Yesu mwenyewe ametufundisha.
  Yesu mwenyewe amefumbulia.
  Neno la Mungu nani atakana?
 5. Sogea meza yake takatifu,
  Kwa moyo safi nawe umpokee,
  Atatolea nyingi zake neema
 6. Mungu mwamini, nakutumaini,
  Ee Mungu mzima, ninakushukuru,
  Ee Mungu wangu, nakupenda sana
 7. Sadiki, mkristu, upate wokovu
  Ndiyo ahadi ya Mwenyezi Mungu,
  Mwisho mbinguni atakupokea
Ukaristia ni Yesu
CATEGORYEkaristia (Eucharist)
 • Comments