Unirehemu Unitakase

Unirehemu Unitakase
Alt TitleNitalisifu Nitalihimidi
ChoirTBA
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
Composer(traditional)

Unirehemu Unitakase Lyrics

 1. Nitalisifu nilihimidi jina lako Mungu Mkuu.
  Nitalitunza nilisujudu kwa wema wako ule mkuu

  Unirehemu unitakase, mwisho nifike kwako mbinguni.
  Unirehemu unitakase, mwisho nifike kwako enzini.

  Nitalisifu nilihimidi . . .
 2. Umeyalinda maisha yangu, nayo maovu kaniepusha.
  Umenilinda nyumbani mwangu, Baraka zako kwangu ni tele.
 3. Kwenye mabonde hata milima, kaniongoza m-chunga wangu.
  Kwenye mashaka na hofu nyingi, kaniepusha we ngome yangu
 4. Nizidishie fadhili zako, kazini mwangu unijalie.
  Unifundishe uniwezeshe, nishukuru kwa sala zangu.
 5. Unijalie rehema zako, nitende wema kwa ndugu zangu.
  Chuki hasira pia ugomvi, niondolee niwe mpole.
 6. Tukufu kwako ee Mungu Baba, mwana na Roho Mtakatifu.
  Ni wewe Alfa pia Omega, mwanzo na mwisho hata milele.
Recorded by St. Paul's Community Choir, Nrb