Login | Register

Sauti za Kuimba

Shangilia Harusi Lyrics

SHANGILIA HARUSI

Yelele lele, yelele lele, leo tunayo furaha tele tele
Twasherehekea arusi ya wenzetu
Wamejitolea kwa moyo wao wote
Twasherehekea yote wametimiza
Arusi leo shangilia aa, shangilieni maarusi hawa
Arusi leo furahia aa, furahieni maarusi hawa

 1. Twaombea baraka zake Bwana
  Munapoanza maisha haya mapya
  Shetani asiwatenganishe kamwe
  Mubaki ndani ya Bwana Mungu wetu
 2. Ewe mwanaume umpende mke wako
  Kwani hiyo ndiyo amri ya Mungu wetu
  Nawe mwanamke umpende mume wakao
  Ndipo ndoa yenu isimame imara
 3. Msiwasahau wazazi wenu pia
  Kwani hao ndio nguzo ya masha yenu
  Watoto wenu na muwatunze vema
  Muwapeleke kwa kanisa ya Bwana
 4. Na sisi sote tulioshuhudia
  Arusi yenu siku hii ya leo
  Twawahimiza mheshimu ndoa yenu
  Kwani ndoa ni sakramenti takatifu

  Yelele lele, yelele lele
  Shangilieni maharusi hawa, furahieni maharusi hawa
Shangilia Harusi
CATEGORYHarusi
 • Comments