Waipeleka Roho Yako

Waipeleka Roho Yako
Performed bySt. Joseph Cathedral Dar-es-Salaam
CategoryRoho Mtakatifu (Pentecoste)
Views6,389

Waipeleka Roho Yako Lyrics

  1. Waipeleka Roho Yako ee Bwana
    Nawe waufanya upya uso wa nchi
    Waipeleka Roho Yako ee Bwana
    Nawe waufanya upya uso wa nchi

  2. Ee nafsi yangu umhimidi Bwana
    Wewe Bwana Mungu wangu umejifanya mkuu sana
    Ee Bwana jinsi yalivyo mengi matendo yako
    Dunia imejaa mali zako
  3. Waiondoa pumzi yao wanakufa
    Na kuyarudia mavumbi yao
    Waipeleka Roho yako wanaumbwa
    Nawe waufanya upya uso wa nchi
  4. Utukufu wa Bwana na udumu milele
    Bwana na ayafurahie matendo yake
    Kutafakari kwangu na kuwe kutamu kwake
    Mimi nitamfurahia Bwana