Uzuri wa Kifo

Uzuri wa Kifo
ChoirKwaya ya Malkia wa Mitume Parokia ya Vincent Palloti Arusha
AlbumDira
CategoryMazishi
ComposerBernard Mukasa
Musical Notes
Timesignature3 8
MusickeyE Major
NotesOpen PDF

Uzuri wa Kifo Lyrics


Basi ndugu zangu, hatimaye imetosha
Acheni kunung'unika kuhusu kifo
Jitayarisheni ili mfe kifo chema
Hiyo hekima ya kweli na ucha Mungu kamili
Kifo ni zawadi ya upendo toka kwa Mungu
Nacho kimeandaliwa kuivuka dunia chungu
Ibada na dini zenu ni upuuzi mtupu
Kama mwisho wake siyo kumfikia Mungu
Lakini hamuwezi kumfikia Mungu
Isipokuwa kwa njia hii ya kifo
1. Dhambi ya Adamu ilimfanya Adamu,
akajificha mbali na uso wa Mungu
Akapewa kifo,
kusudi roho yake irudi karibu na Mungu milele

2. Kifo kilibeba maana yake halisi,
alipoinuliwa Mwokozi wa watu
Akashinda kifo,
kusudi watu wake baada ya kifo warudi kwa Mungu

3. Kama hampendi, taabu za ulimwengu,
kwa nini mwaogopa kujitayarisha
Kupokea kifo,
kusudi muiage dunia mpokee raha ya milele

4. Tofautisheni, kifo nayo mauti,
mauti humpeleka mwenzetu kuzimu
Ingawaje kifo,
humtenganisha mwenzetu na taabu za dunia hii

Favorite Catholic Skiza Tunes

SMS the Skiza ID to 811 to get the song as your Skiza tune.

TitleSKIZA ID
Cha Kutumaini Sina 5814855
Roho Yangu na Ikuimbie 5814859
Nikupe Nini Mungu Wangu 7482438
Sasa Wakati Umefika 7482439
Zaeni Matunda Mema 5814860
Nitakwenda Mimi Mwenyewe 7482440
Huniongoza Mwokozi 5814856
Bwana Kama Wewe Ungehesabu Maovu Yetu 7482444
Utukuzwe Ewe Baba 7482441
Tazama Tazama 7482442