Login | Register

Sauti za Kuimba

Upendo na Ukarimu Lyrics

UPENDO NA UKARIMU

@ Bernard Mukasa

 1. Watu wengi tunajaribu upendo
  Tunawajali wale wanaotuhusu
  Tunaojua wataweza kutulipa
  Hatuwathamini wale wasiotuhusu
  Wala wasiojiweza, lakini

  {Leo tumejifunza wote,
  upendo ni kitu gani (wapendwa)
  Tena tumepewa mfano,
  ukarimu una sifa gani (wapenzi) } * 2

 2. Tunawakopesha wenye kipato kikubwa
  Tukiamini nao watatukopesha
  Wakitujia wenye shida na fukara
  Tunawakimbia eti hawakopesheki
  Na wana madeni mengi, lakini
 3. Wakiugua wenye nafasi za juu
  Tunajazana kwao na vichupachupa
  Tukiamini na sisi tukiugua
  Watalundikana kwetu na vifuko fuko
  Kadi na michango mingi, lakini
 4. Tukitembelewa na mtu mwenye viraka
  Tunauliza kama tulimualika
  Akija aliyeshuka kwenye shangingi
  Tunamwuliza kinywaji anachokunywa
  Tena kwa unyenyekevu lakini
Upendo na Ukarimu
COMPOSERBernard Mukasa
CATEGORYLove
SOURCETanzania
 • Comments