Mbona Mmegeuka Lyrics

MBONA MMEGEUKA

@ Bernard Mukasa

Mlipokea nguvu ya Mungu ya kushinda tamaa
Siku ile mlipobatizwa,
Mkaahidi kumkataa, Ibilisi na vyake,
Sasa vipi muwe wabinafsi
Hamshibishwi kwa riziki yenu,
Aliyowapimia Mungu wenu
Mnatafuna riziki ya hao walio wadogo
Mnakula rushwa ndugu zangu

 1. Uhai na nguvu mlivyojaliwa, si kwa ajili yenu,
  Ni kwa ajili ya wahitaji
 2. Elimu mliyoipata wapendwa, si utukufu wenu
  Akatukuzwe Muumba wenu
 3. Fedha navyo vyeo mlivyoazimwa
  Jembe la Mungu wenu, mkatumikie shamba lake
 4. Acheni umimi acheni ulafi, ingawa kuna leo
  Kumbuka kwamba na kesho ipo
 5. Kipimo mnachowawia wadogo, hicho kitatumika
  Usoni penu siku ya mwisho
Mbona Mmegeuka
ALT TITLEMlipokea Nguvu ya Mungu
COMPOSERBernard Mukasa
CATEGORYTafakari
 • Comments