Login | Register

Sauti za Kuimba

Wateule wa Bwana Lyrics

WATEULE WA BWANA

@ Stanslaus Mujwahuki

{Wateule wa Bwana, Karibuni mezani pake, njooni
Bwana awaalika enyi wenye moyo safi} *2

{Amewaandalia, leo, karamu takatifu
Mwili na damu yake chakula safi cha roho} *2

  1. Kwanza tuzitakase nafsi zetu wenyewe
    Tukisha kutakasa, tuje mbele zake
  2. Karibuni mezani, Bwana awaalika
    Kwenye karamu yake, enyi wenye moyo safi
  3. Na tule mwili wake, na tunywe damu yake
    Ndicho chakula bora, cha rohoni karibuni
Wateule wa Bwana
COMPOSERStanslaus Mujwahuki
CHOIRShirikisho la Kwaya Katoliki Dsm (Shikwaka)
ALBUMKaribu Tanzania
CATEGORYEkaristia (Eucharist)
  • Comments