Ni Kweli Amezaliwa Lyrics

NI KWELI AMEZALIWA

@ A. Liampawe

Ni kweli amezaliwa Mkombozi wetu Masiha
Malaika wanaimba kwa furaha wakimsifu Bwana
{Na sisi tunafurahia Mkombozi wetu kazaliwa
Na utumwa umetutoka aleluya tushangilie } *2

 1. Kwenye mji wa Daudi Mkombozi kazaliwa
  Wote twende tukamwone amelazwa manyasini
 2. Tuna haki kufurahi tumepata Mkombozi
  Amekuja tukomboa hivyo wote tufurahi
 3. Utukufu juu Mbinguni, na amani duniani
  Kwa watu wote wenye mapenzi mema aleluya
 4. Bwana Yesu kazaliwa, amekuja tukomboa
  Katuletea wokovu, hivyo tuimbe aleluya
Ni Kweli Amezaliwa
COMPOSERA. Liampawe
CATEGORYNoeli (Christmas Carols)
SOURCETanzania
 • Comments