Moyo Wangu Wamwadhimisha Bwana Lyrics

MOYO WANGU WAMWADHIMISHA BWANA

Moyo wangu wa mwadhimisha Bwana
Roho yangu yamfurahia Mungu

 1. Ni kwa kuwa ameutazama
  unyonge wa mjakazi wake
 2. Kwa maana tazama tokea sasa
  Vizazi wataniita mbarikiwa
 3. Kwa kuwa amenitendea mambo makuu
  Na jina lake takatifu kweli
 4. Ameyatenda maajabu
  na jina lake takatifu
 5. Wamchao hudumisha rehema
  Vizazi hata na vizazi
 6. Amefanya nguvu kwa mkono wake
  Atawanya wote wenye kiburi
 7. Aangusha wakuu wa enzi
  Na wanyonge yeye huwakweza
 8. Wenye njaa amewashibisha mema
  Walio na mali aondoa tupu
 9. Amemsaidia mtumishi wake
  Ili kukumbuka rehema zake
 10. Utukufu kwao Baba na Mwana
  Msaada wa Roho Mtakatifu
 11. Kama ulivyokuwa hapo mwanzo
  Ni vivyo sasa hata milele
 12. Utukufu kwa Baba na Mwana kwa Roho
  Kama vile mwanzo wa hata milele Amina
Moyo Wangu Wamwadhimisha Bwana
CATEGORYBikira Maria
REFMagnificat
SOURCETanzania
 • Comments