Login | Register

Sauti za Kuimba

Litukuzeni Jina Lyrics

LITUKUZENI JINA

@ Fr. G. F. Kayeta

 1. Litukuzeni Jina la Mungu daima milele
  Enyi mataifa, mshangilieni Mungu wetu
  Kwa kuwa Bwana ni Mtukufu wa kutisha
  Yeye ni mfalme mkuu wa dunia yote
  Sifuni Bwana kwa shangwe

  {Jina la Mungu lihimidiwe daima milele
  ( litukuzwe litukuzwe litukuzwe litukuzwe litukuzwe litukuzwe)
  Enyi mataifa mhimidini
  Kwa kuwa fadhili zake (kwetu sisi) zadumu daima milele } *2

 2. Jina lake Bwana litukuzwe sasa hata milele
  Viumbe vya Bwana Sifuni Bwana Mungu wetu
  Toka mawio hata machweo ya jua
  Sifuni jina lake Bwana Mungu wetu
  Sifuni Bwana Mwenyezi
 3. Enyi watumishi sifuni Bwana kutoka Mbinguni
  Mbingu nanyi maji, lisifuni jina la Bwana
  Wafalme wa dunia nanyi watu wote
  Wakuu nanyi wakaazi wote wa dunia
  Sifuni Bwana Mwenyezi
Litukuzeni Jina
COMPOSERFr. G. F. Kayeta
CATEGORYThanksgiving / Shukrani
MUSIC KEYC Major
TIME SIGNATURE4
4
SOURCETanzania
NOTES Open PDF
 • Comments