Yesu Yupo

Yesu Yupo
ChoirTBA
CategoryTBA
ComposerBernard Mukasa
SourceTabora Tanzania

Yesu Yupo Lyrics

Yakija mawimbi hata dhoruba ikizidi
Nakanyaga maji nasogea Bwana Yesu
Upepo mkali hata bahari ichafuke
Nakanyaga maji nasogea Bwana Yesu

 1. Ni yeye Yesu alitembea juu ya maji (sikia)
  Akamuita Petro ashuke akamfuate
  Na hata Petro alipojawa na wasiwasi (sikia)
  Yesu akawa pamoja naye na kutulia
 2. Nami ninayaacha niyasafiri nayo (sikia)
  Nashuka nikamfuate Yesu niende naye
  Nijapopatwa na misukosuko katikati (sikia)
  Sitateteleka kwani Yesu yu pamoja nami
 3. Nitayatimiza yote atakoyonipa
  Yesu ni wangu nami ni wa Yesu najivunia