Login | Register

Sauti za Kuimba

Ee Baba Pokea Sadaka Lyrics

EE BABA POKEA SADAKA

@ G. Hyera

{ Ee Baba pokea sadaka yetu tunayokutolea
Hiyo ni kazi ya mikono yetu wanadamu } *2
{Twakuomba uipokee, ee Bwana uibariki
Bwana sadaka hii tunayokutolea } *2

  1. Mkate pia divai tunakutolea
    Upokee utakase na ubariki
  2. Na mazao ya mashamba Baba upokee
    Ni zawadi ya mavuno kwa mikono yetu
  3. Nyoyo zetu tunakupa zote mali yako
    Na fedha zetu tunaleta, Baba zipokee
Ee Baba Pokea Sadaka
COMPOSERG. Hyera
CHOIRSt. Cecilia Mwenge Dsm
ALBUMViuzeni Mlivyo Navyo
CATEGORYOffertory/Sadaka
SOURCEDar-es-Salaam Tanzania
  • Comments