Login | Register

Sauti za Kuimba

Tutoe Sadaka Lyrics

TUTOE SADAKA

@ V. B. Kanuti

Tutoe sadaka kwa Bwana na Mungu wetu kwa heshima
Tumtolee Bwana shukrani zetu
Katoe kwa moyo thabiti katoe ulicho nacho
Naye Bwana Mungu wako naye Bwana atakubariki

 1. Enyi waumini tutoe sadaka kwa Mungu wetu
  Tutoe sadaka kwa moyo wa upendo
  Tunzo letu kubwa huko Mbinguni
 2. Njooni wote tutoe sadaka zetu kwake Bwana
  Kwa sifa na utukufu wake Mungu wetu
  Kwa shukrani tukampe Bwana
 3. Enyi wakristu fikirini mema ametutendea
  Nasi kwa shukrani tumpe Bwana kama zawadi
  Naye atazidi kutujalia
Tutoe Sadaka
COMPOSERV. B. Kanuti
CATEGORYOffertory/Sadaka
SOURCEDar-es-Salaam Tanzania
 • Comments