Hazina ya Mvivu Lyrics

HAZINA YA MVIVU

@ J. Matthias

Hazina ya Mvivu ni maneno ya uongo (na tena)
Furaha ya mvivu ni kugombanisha watu

 1. Hawezi kulala kapata usingizi usiku
  Usiku mzima hukodoa macho akiwaza
  Kukipambazuka aende kwa nani kupiga umbeya
 2. Asubuhi mapema huamka na kuvaa nguo
  Hajafagia nyumba huyo huyo kwa jirani kaenda
  Hodi jirani jirani naye karibu tupo unasemaje
  Atapiga umbea hapo hadi chakula cha mchana ale
 3. Akipitapita mitaani huwa amependeza
  Salamu kwa watu utasema huyu ni mtu mwema
  Kumbe ni muovu asiye kuwa na aibu kwa watu
 4. Wenzake wanaamka mapema na kwenda kazini
  Yeye akiamka huyo huyo safari kwenye pombe
  Akishafika huko tazama anavyolewa wala hawazi
  Familia yake itakula nini mchana na usiku
Hazina ya Mvivu
COMPOSERJ. Matthias
CHOIRSt. Anna Old Maswa Bariadi Shinyanga
ALBUMOna Wanadamu wa Leo
CATEGORYTafakari
SOURCEShinyanga Tanzania
 • Comments