Nalisema Nitayakiri Maasi Yangu

Nalisema Nitayakiri Maasi Yangu
Performed by-
CategoryZaburi
ComposerJohn Mgandu
Views6,422

Nalisema Nitayakiri Maasi Yangu Lyrics

  1. Nalisema nitayakiri maasi yangu ee Bwana
    Nawe ukausamehe upotovu wa dhambi yangu
    Nawe ukausamehe upotovu wa dhambi yangu

  2. Heri aliyesamehewa dhambi na kusitiriwa makosa yake
    Heri Bwana asiyemhesabia upotovu
  3. Nalikujulisha dhambi yangu
    Wala sikuuficha upotovu wangu
  4. Ndiwe sitara yangu utanihifadhi na mateso
    Utanizungushia nyimbo za wokovu
  5. Naye mtu mwovu ana mapigo mengi
    Bali amtumainiaye Bwana fadhili zinamzunguka