Mungu Wangu Mungu Wangu Mbona Umeniacha

Mungu Wangu Mungu Wangu Mbona Umeniacha
ChoirTBA
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
SourceTanzania

Mungu Wangu Mungu Wangu Mbona Umeniacha Lyrics

Mungu wangu, Mungu wangu mbona umeniacha

 1. Wote wanionao huncheka sana
  Hunifyonya watikisa vichwa vyao husema
  hutegemea Bwana na amponye
  Na amwokoe sasa maana apendezwa na yeye
 2. Kwa maana mbwa wamenizunguka
  Kusanyiko la waovu wamenisonga
  Yamenizua mikono na miguu
  Naweza kuihesabu mifupa
 3. Wanagawanya nguo zangu
  Na vazi wanalipigia kura
  Nawe usiwe mbali
  Ee Mungu wangu fanya haraka kunisaidia
 4. Nitalihubiri jina lako kwa ndugu zangu
  Katikati ya kusanyiko nitakusifu
  Ninyi mnaomcha Bwana, msifuni
  Enyi nyote mlio wazao wa Yakobo mtukuzeni.