Yesu Mwana wa Mungu

Yesu Mwana wa Mungu
ChoirTBA
CategoryPasaka (Easter)
Composer(traditional)
SourceTanzania
Musical Notes
Time Signature2
4
Music KeyG Major

Yesu Mwana wa Mungu Lyrics

Yesu Mwana wa Mungu * 2 Leo amefufuka
Piga vigelegele *2 leo amefufuka

 1. Yesu Mwana wa Mungu kweli amefufuka
  Ahadi yatimia mzima amefufuka
 2. Kristu mshindaji, mkubwa ametupatanisha
  Na babaye Mbingunikwa damuye azizi

  Kristu mwanakondoo amechinjwa sadaka
  Tuile karamuye tuimbe aleluya
 3. Kristu mchingaji mwema alitoa maisha
  Kwa ajili ya kondoo mzima amefufuka
 4. Kristu aliuawa katika udhaifu
  Anaishi daima kwa nguvu yake Mungu
 5. Nendeni duniani kahubiri Injili
  Wote wabatizwao Mbingu watauridhi
 6. Nitawahubiria ndugu zangu daima
  Jina lako tukufu nitakusifu sana
 7. Leo ndiyo siku kuu ilifanywa na Mungu
  Umefufuka Mbingu kwa ushindi wa Yesu