Wastahili Kusifiwa Lyrics

WASTAHILI KUSIFIWA

@ G. A. Miyombo

{Wastahili, wastahili kusifiwa ee Bwana
kusifiwa na kutukuzwa na viumbe vyako }*2

Mbingu na dunia zimejaa sifa zako, sifa zako ee Bwana *2
{Pokea masifu ya viumbe vyako - uhimidiwe milele aleluya
Bwana wa mabwana - uhimidiwe - uhimidiwe milele aleluya }*2

  1. Malaika mbinguni wanakuhimidi wewe wakusifu milele, ee Bwana
  2. Milima na mabonde, miti yote ya porini vyakusifu milele, ee Bwana
  3. Wanyama wa porini na wanyama wafugwao wakusifu milele, ee Bwana
  4. Samaki baharini nao ndege wa angani wakusifu milele, ee Bwana
Wastahili Kusifiwa
COMPOSERG. A. Miyombo
ALBUMKanisa Linalosafiri
CATEGORYGeneral
  • Comments