Yesu Ateswa Msalabani

Yesu Ateswa Msalabani
ChoirTBA
CategoryTBA
ComposerFr. G. F. Kayeta
SourceDar-es-salaam Tanzania

Yesu Ateswa Msalabani Lyrics

 1. Tunapoona Bwana Yesu kuteswa msalabani
  Tunasikitika kweli
  Kwani tumekusulubu ee Bwana utuhurumie
 2. Dhambi zetu nyingi sana asili ya mateso
  Watupenda mpaka mwisho
  Umekufa tuokoke ee Bwana utuhurumie
 3. Tunapona msalabani sawa na mwizi mbaya
  Ulitaka kutukanya
  Tuyaache majivuno, ee Bwana utuhurumie
 4. Tunapoona msalabani miiba yachoma kichwa
  Unalipa kwa matesa
  Fungua na tamaa zetu ee Bwana utuhurumie
 5. Msalabani, umefungwa na mikono ya damu
  Mkono wako wenye heri
  Utujaze na baraka, ee Bwana utuhurumie
 6. Mwili wote wafunikwa, na damu ivujayo
  Damu yako isafishe
  Uovu wote wa rohoni, ee Bwana utuhurumie
 7. Moyo wako umetonwa, mlango sasa wazi
  Tutakase tuingie,
  Tukae moyoni mwako, ee Bwana utuhurumie