Ewe Mama Maria Umebarikiwa

Ewe Mama Maria Umebarikiwa
Performed by-
CategoryTBA
Views2,709

Ewe Mama Maria Umebarikiwa Lyrics

  1. {Ewe Mama Maria umebarikiwa,
    Mama mwenye huruma, utuombee} *2

  2. Umebarikiwa Mama wa Mungu
    Mama wa Mwokozi Mama wa Yesu
    Utuombee Mama mwenye huruma
  3. Uwinguni juu unapoketi
    Na mwanao Yesu anatawala
    Utuombee Mama utuongoze
  4. Adui shetani ametubana
    Utukinge na hila zake
    Utuombee mama mwenye huruma
  5. Na siku ya mwisho usiwe mbali
    Kufa peke yetu sikubali
    Mama mwenye huruma utuombee
  6. Mama wetu bora tunakusifu
    Na huko Mbinguni wakuheshimu
    Utuunganishe ee Mama mwema