Login | Register

Sauti za Kuimba

Twausifu Moyo wako Maria Lyrics

TWAUSIFU MOYO WAKO MARIA

Twausifu, moyo wako Mama Maria, (moyo mwema )
Twauheshimu, moyo wako mama Maria (moyo safi)
Moyo wako Maria usio na doa
Moyo wako Maria usio na doa

 1. Moyo wako Mama una faraja
  Unang'ara sana unavyopendeza
  Moyo wako Mama mpenzi Maria
  Ni msafi kweli unameremeta
 2. Moyo wako mama, umekingiwa
  Dhambi ya asili tuliyoirithi
  Moyo wako mama ni mtakatifu
  Umejaa neema neema teletele
 3. Moyo wako mama, kama waridi
  Unafurahisha unametameta
  Moyo wako mama, kama dhahabu
  Ing'arayo sana mfano wa kioo
 4. Moyo wako mama, ni mtii sana
  Moyo wako mama mtulivu kabisa
  Moyo wako mama ni nuru njema
  Ituongozayo kufika Mbinguni
 5. Moyo wako mama, ni mnyenyekevu
  Moyo wako mama una heri tele
  Moyo wako mama ni wa amani
  Moyo wako mama una neema ya Mungu
 6. Tuombee mama yetu Maria
  Tuombee mama kwa mwanao Yesu
  Ili atakase mioyo yetu
  Ifanane nawe mama yetu mpenzi
Twausifu Moyo wako Maria
CHOIRKwaya ya Moyo Safi wa Bikira Maria, Unga Limited Arusha
ALBUMUwe Nasi Mama Maria
CATEGORYBikira Maria
SOURCEArusha Tanzania
 • Comments