Kwa Nini Wasimama Mbali

Kwa Nini Wasimama Mbali
ChoirSt. Maurus Kurasini
AlbumHubirini Kwa Kuimba
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
ComposerD. Mlolwa
SourceTanzania
VideoWatch on YouTube
Musical Notes
Time Signature3
8
Music KeyA Major
NotesOpen PDF

Kwa Nini Wasimama Mbali Lyrics

Bwana ee Bwana, kwa nini wasimama mbali
Ee Bwana ee Bwana, kwa nini wasimama mbali
{ Kwa nini kujificha na kujificha nyakati za shida
Kwa nini kujificha Bwana nyakati za shida } *2

 1. Kwa kiburi chake mtu asiye haki
  Mnyonge anafuatiwa anafuatiwa kwa ukali
  Na wanaswe kwa hila hizo hizo walizoziwaza
 2. Maana mdhalimu, mdhalimu hujisifia
  Hujisifia sifia tamaa ya nafsi yake
  Na mwenye uchoyo humkataa Bwana na kumdharau
 3. Asema moyoni mwake, asema sitaondoshwa
  Kizazi hata kizazi, sitakuwamo taabuni
  Kinywa chake kimejaa laana na hila na dhuluma