Sogeeni Kwa Karamu

Sogeeni Kwa Karamu
ChoirSt. Maurus Kurasini
AlbumHubirini Kwa Kuimba
CategoryEkaristia (Eucharist)
SourceTanzania

Sogeeni Kwa Karamu Lyrics

 1. Bwana Yesu ni mwili wa uzima, tukila tutashibishwa
  Bwana Yesu ni damu ya uzima, Yeye ni uzima

  Sogeeni kwa karamu ya upendo
  Twende sote tule mwili wake
  Twende sote tunywe damu yake Bwana tupate uzima

 2. Tunapokula mwili wake Bwana, na kuinywa damu yake
  Tunatangaza kifo chake Bwana Mpaka arudipo
 3. Alaye mwili wake Bwana wetu, na kuinywa damu yake
  Akila bila ya kustahili anajihukumu