Njooni Tushukuru Lyrics

NJOONI TUSHUKURU

@ Victor Aloyce Murishiwa

 1. Watu wote njooni tushukuru, njooni tushukuru aee,
  Simameni tuseme asante, tuseme asante aee

  {Na tuimbe - kwa vigelegele
  Na tucheze - ngoma na vinanda
  Kwa vinubi, zeze na filimbi aee } *2

 2. Yeye ndiye aliyeziumba, mbingu na dunia aee
  Vitu vyote vionekanavyo, na visivyoonekana
 3. Kwa mfano wake katuumba, tufanane naye aee
  Ametupa vyote tutawale, tumtumikie aee
 4. Shukuruni Mungu wa miungu, Bwana wa mabwana aee
  Zitoeni dhabihu za shangwe, za kumshukuru aee
 5. Tukuzeni Mungu siku zote, daima milele aee
  Msifuni kwa kila sauti hata kwa ukimya aee
Njooni Tushukuru
COMPOSERVictor Aloyce Murishiwa
ALBUMTuchome
CATEGORYThanksgiving / Shukrani
SOURCEDar-es-Salaam Tanzania
 • Comments