Hata Ndimi Elfu Lyrics

HATA NDIMI ELFU

 1. Hata ndimi elfu, hazitoshi kweli
  Bwana Yesu kumsifu kwa zake fadhili
 2. Yesu jina kubwa liwezalo kufukuza hofu,
  linafurahisha hili lanipa wokovu
 3. Jina hili ni uzima, ni afya amani ,
  Laleta habari njema, twalipiwa deni.
 4. Yesu huvunja mikufu ya dhambi moyoni,
  Msamaha ,tena nguvu twapata rohoni
 5. Kwa sauti yake vile, watu hufufuka,
  Wakafurahi milele pasipo mashaka
Hata Ndimi Elfu
CATEGORYTafakari
 • Comments