Chakula cha Bwana Sasa Kiko Tayari

Chakula cha Bwana Sasa Kiko Tayari
ChoirTBA
CategoryEkaristia (Eucharist)
ComposerF. A. Nyundo

Chakula cha Bwana Sasa Kiko Tayari Lyrics

 1. Chakula cha Bwana, sasa kiko tayari ndugu
  Karibuni karibuni twende kumpokea
  Nacho kimeshuka kimetoka Mbinguni ndugu
  Karibuni karibuni twende kumpokea

  Bwana Yesu anatuita twende
  Tukale mwili wake
  Tukanywe damu yake
  Sote twende tukampokee

 2. Tumekaribishwa kumpokea Mwana kondoo
  Karibuni karibuni twende kumpokea
  Anayeondoa dhambi zote za ulimwengu
  Karibuni karibuni twende kumpokea
 3. Bwana ndiye njia, ya Mbinguni tukampokee
  Karibuni karibuni twende kumpokea
  Atuita kwake kula mwili na damu yake
  Karibuni karibuni twende kumpokea