Login | Register

Sauti za Kuimba

Mimi Ndimi Chakula Lyrics

MIMI NDIMI CHAKULA

@ V. B. Kanuti

Mimi ndimi chakula cha uzima
Chakula cha uzima
{Aulaye mwili wangu, na kuinywa damu yangu
Huyo anao uzima wa milele } *2

 1. Mimi ndimi chakula cha uzima
  kilichoshuka kutoka mbinguni
  Alaye chakula hiki ataishi milele
 2. Chakula nitakachowapa mimi
  Ni mwili wangu pia na damu yangu
  Ni kwa ajili ya uzima wa ulimwengu
 3. Aulaye mwili na damu yangu
  Huyo ana uzima wa milele
  Nami nitamfufua siku ya mwisho
Mimi Ndimi Chakula
COMPOSERV. B. Kanuti
CATEGORYEkaristia (Eucharist)
 • Comments