Je Bwana Nastahili Lyrics

JE BWANA NASTAHILI

@ G. M. Liheta

Je Bwana nastahili kujongea meza yako?
Je Bwana nastahili kujongea meza yako?
Kwani mimi si mnyofu wa moyo nifanye nini
Bwana ninatamani Nifanye nini
nami nijongee meza yako Bwana nipate uzima wa milele

 1. Njooni kwangu nyote, msiogope
  Njooni mimi ni uzima wa milele
 2. Njoo mwenye njaa usiogope
  Mwili wangu ni chakula cha uzima
 3. Njoo mwenye kiu usiogope
  Damu yangu ni kinywaji cha uzima
 4. Njoo mwenye dhambi usiogope
  Kwani mimi ni wokovu wa milele
Je Bwana Nastahili
COMPOSERG. M. Liheta
CHOIRSt. Antony of padua Magomeni
ALBUMTwende Mezani
CATEGORYEkaristia (Eucharist)
SOURCETanzania
 • Comments