Furaha ya Ajabu

Furaha ya Ajabu
Performed by-
CategoryHarusi
Views3,602

Furaha ya Ajabu Lyrics

  1. Furaha ya ajabu, pia na vigelegele,
    kwa hao ndugu zetu, wanaoona.
    Wanathibitisha kuwa wataishi kama mke na mme *2

    Mmethibitisha mbele ya kanisa
    ya kwamba mtaishi na mkipendana
    Siku zote daima na milele
    Tunawatakia amani ya Bwana
    na upendo wake ukae na nyinyi
    Siku zote daima na milele

    (Tenor) Mmeahidi
    All Mmeahidi kwamba mtaishi
    (Tenor) Katika mema
    Katika mema na katika mabaya

    (Tenor) Mmeahidi
    All Mmeahidi kwamba mtaishi
    (Tenor) Kwa utajiri
    Kwa utajiri na umaskini
    (Tenor) Mmeahidi
    All Mmeahidi kwamba mtaishi
    (Tenor) Mpaka kifo
    Mpaka kifo kitakapowatenga
  2. Mmepewa pete ya kuwa ni ukumbusho alama ya ahadi ya ndoa yenu
    Ya kwamba mtaishi na mkipendana mpaka kifo chenu *2

    Mmethibitisha mbele ya kanisa ya kwamba mtaishi na mkipendana
    Siku zote daima na milele
    Tunawatakia amani ya Bwana na upendo wake ukae na nyinyi
    Siku zote daima na milele