Yu Mwangu kweli Mungu

Yu Mwangu kweli Mungu
ChoirTBA
CategoryTBA
Composer(traditional)
SourceTanzania

Yu Mwangu kweli Mungu Lyrics

 1. Yu mwangu kweli Mungu a, yu nami si uongo,
  Naye mamoja nangu a, niliye mdude mdogo,
  Ee Rabbi nakuungama, ndiwe mkombozi wangu
  Mwenyezi, mwenezi, mtoaji wa neema
  Mwenyezi, mwenezi, mtoaji wa neema
 2. Na haya kwani mdhambi mno, nawe mtukufu
  Ee mambo yasiyo mfano, mpenda utakatifu
  Nakuabudu mi mjao, tayari masikanio
  Kwenenda, kutenda, kwa kila amriyo
  Kwenenda, kutenda, kwa kila amriyo
 3. Walakini mi mdhaifu, kusema sikufanya
  Hivyo nilivyo mkosefu, hata naona haya
  Ee Rabbi wezesha moyo, wangu hutia neemayo
  Utake, ushike, yote mapenziyo
  Utake, ushike, yote mapenziyo