Sadaka ya Kuazima

Sadaka ya Kuazima
Alt TitleJiandae Kutoa Sadaka
Performed by-
CategoryOffertory/Sadaka
ComposerMartin M. Munywoki
Views3,462

Sadaka ya Kuazima Lyrics

  1. Jiandae wiki nzima weka tayari
    sadaka yako mkristu (toa kwa moyo safi)
    Usitoe kwa uchoyo wala sadaka ya kuazima
    {(jasho lako) umtolee Mungu alicho kupa hahitaji zaidi
    (maana) Vitu vyote mali yake toa kwa ukarimu } *2

  2. Ninaona hasara kutoa (nanung'unika)
    Bwana ona mi nilivyo changanyikiwa
    Mara nyingi naomba jirani (hapa kitini)
    siyo yangu ni sadaka ya kuazima
  3. Ninaona uchoyo kutoa (sadaka yangu)
    ninaleta kidogo tena kwa uchungu
    Mara nyingine sitoi kitu (nilicho nacho)
    ninaficha sadaka yangu mfukoni
  4. Ninaona aibu kubaki (ni wasiwasi)
    nimeketi nao wengine wanatoa
    Mara nyingine hata siendi (nimekimbia)
    kanisani ninahepa michango nyingi
  5. Wana baraka wanaotoa (kwa moyo ule )
    wa Abeli wa Ibrahimu na Isaka
    Bwana Mungu haipendi sadaka (yake Kaini)
    wala yule Anania na Safira