Login | Register

Sauti za Kuimba

Kaeni Katika Pendo Lyrics

KAENI KATIKA PENDO

@ Stanslaus Mujwahuki

Kama vile Baba alivyonipenda mimi
Nami nilivyo wapenda ninyi
Kaeni katika pendo langu
Kaeni - katika pendo (langu) * 2
Kaeni katika pendo langu

 1. Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu
  Kama vile mimi nilivyozishika, amri za Baba yangu
  Na kukaa katika pendo lake
 2. Hayo nimewaambia, ili furaha yangu iwe ndani yenu
  Na furaha yenu itimizwe
 3. Amri yangu ndiyo hii, mpendane kama nilivyowapenda
  Kama nilivyowapenda ninyi
 4. Hamna aliye na upendo, upendo mwingi kuliko huu
  Wa mtu kutoa uhai wake, kwa ajili ya rafiki zake
Kaeni Katika Pendo
COMPOSERStanslaus Mujwahuki
CATEGORYLove
MUSIC KEYD Major
TIME SIGNATURE6
8
SOURCEMsimbazi Dsm
NOTES Open PDF
 • Comments