Login | Register

Sauti za Kuimba

Siri ya Moyo Wangu Lyrics

SIRI YA MOYO WANGU

@ Bernard Mukasa

{Siri ya moyo wangu, ni kilio changu
Na kilio cha moyo wangu, niione huruma yako } *2
Mungu wangu kinga yangu, nakuita Bwana
Ukinigeuka wewe nimekwisha mimi
Wewe ndiwe fimbo yangu, kimbilio langu
Ndiwe boma la wokovu, msaada wangu
Niepushie makucha ya dunia

 1. Kikombe cha uchungu nimekunywa kwa harakwa
  Sasa kimenikwama
  Nimenaswa nimefikwa yamenikuta mimi
  Ee Bwana ninakuita mimi ee Mungu njoo unikamilishe
 2. Najua haina thamani, sala yangu ni chafu
  Ibada haifai
  Nimkimbilie nani zaidi yako wewe
  Naililia huruma yako, mkono wako nishike Bwana
 3. Mimi sistahili kabisa kupokea neema
  Kutoka kwako Bwana
  Ni mchafu ni mdhambi, nimeoza moyoni
  Mikono nakuinulia Bwana, machozi yangu nafukia mimi
Siri ya Moyo Wangu
COMPOSERBernard Mukasa
CHOIRSt. Kizito Makuburi
CATEGORYTafakari
 • Comments