Angalieni Msifanye Wema

Angalieni Msifanye Wema
ChoirSt. Francis of Assisi Msimbazi
CategoryOffertory/Sadaka
ComposerStanslaus Mujwahuki

Angalieni Msifanye Wema Lyrics

 1. Angalieni msifanye wema wenu,
  Msifanye wema wenu machoni mwa watu,
  Ili mtazamwe nao,
  Kwa maana, mkifanya hivyo hampati
  dhawabu kwa baba yenu aliye Mbinguni

 2. Basi wewe utoapo sadaka,
  Usipige panda mbele yako,
  Kama wanafiki wafanyavyo,
  katika masinagogi na njiani,
  Ili watukuzwe na watu.
 3. Amin amin nawaambieni,
  Wamekwisha pata dhawabu yao,
  Bali wewe utoapo sadaka,
  Hata mkono wako wa kushoto usijue,
  Ufanyalo mkono wako wa kuume.