Login | Register

Sauti za Kuimba

Asubuhi Imefika Lyrics

ASUBUHI IMEFIKA

Asubuhi imefika sasa, usiku umeisha, kumeshapambazuka
Na mchana umewadia, usiku umeisha, kumeshapambazuka
Ikawa ni asubuhi
Viumbe,
Viumbe vyote vishangilie pilka za hapa na pale
Kwa kuwa Mungu aliye hai ametulinda
Tushangilie tuimbe, kwa furaha tuimbe
Kwa kuwa Bwana ni mwema tumwimbie kwa maringo

 1. Nguvu tumejaliwa tumeamka na afya njema
  Mungu ametulinda tumeona siku ya leo
  Hivyo basi tumshukuru Muumba
 2. Nyota zilikuwepo usiku huu wa manene
  Wote tumefumbwa jua tumelala usigizi
  Hivyo basi tumshukuru Mwenyezi
Asubuhi Imefika
CATEGORYThanksgiving / Shukrani
 • Comments