Tu Mavumbi Sisi

Tu Mavumbi Sisi
ChoirKwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)

Tu Mavumbi Sisi Lyrics

 • { Siku zinapita, miaka yapita
  Neno lake Bwana halitapita kamwe }*2
 • Tu mavumbi sisi, tutarudi mavumbini *2
 • mmmm mmmm mmm siku hiyo ni ya huzuni mno
  mmmm mmmm mmm siku hiyo kweli inatisha
 • Kwa maana siku hiyo,
  Mavazi yako yatakuwa ni sanda
  Kitanda chako kitakuwa jeneza
  Na nyumba yako iyakuwa kaburi
  Jamaa zako watakutupia udongo,
  kwa heri ya milele!
 • { Roho ndiyo roho ndiyo itiayo uzima
  Mwili haufai kitu } * 2
 • Tu mavumbi sisi, tutarudi mavumbini
 • Tazameni mimea, shambani
  Matunda na maua, vyapendeza
  Vyote vitanyauka
  Wanyama wa pori, na nyumbani
  Na ndege angani, wapendeza
  Wote wataangamia
 • Ee ndugu sasa utubu rudi
  Mrudie Mungu wako
  Kwa maana duniani sisi ni wasafiri
  Hujui saa na siku ndugu ya kuiacha dunia
  Kwa maana duniani sisi ni wasafiri
 • Sayari angani zapendeza
  Mito na mabonde duniani
  Vyote vitatokomea
  Mungu ndiye peke ajuaye
  Siri ya maisha ya viumbe
  Vyake ulimwenguni
 • { Siku zinapita, miaka yapita
  Neno lake Bwana halitapita kamwe }*2
  Tu mavumbi sisi, tutarudi mavumbini * 2