Bwana Yesu Twakumbuka

Bwana Yesu Twakumbuka
ChoirKwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha
AlbumHii ni Kwaresma
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)

Bwana Yesu Twakumbuka Lyrics

BWANA YESU TWAKUMBUKA

 1. Bwana Yesu twakumbuka
  Mateso yako makuu
  Ili utuokoe sisi
  Bustanini Getsemani
  Uchungu ukakupata
  Ukikumbuka dhambi zetu

  Taji la miiba wavikwa
  Na mijeredi wapigwa
  Ni mateso gani hayo
  Jasho la damu latona
  Mwili mzima ni mateso
  Yote yo kwa ajili yetu
 2. Kwa Pilato unafika
  Bure unashtakiwa
  Umekosa nini wewe Yesu
  Sisi twasitahili hukumu
  Sio wewe Bwana Yesu
  Ndiyo sisi siyo wewe

  Msalaba ni mzito
  Umeshinda nguvu zako
  Hata chini waanguka
  Askari wakupiga
  Tena bila ya huruma
  We uliye muumba wao
 3. Njiani unaonana
  Na mamayo Maria
  Mwilio wajaa madonda
  Kwa uchungu Mama MAria
  Alipomwona mwanaye
  Machozi yalimtoka

  Huku na huku wakuvuta
  Wauwaji hawa wabaya
  Kwa nguvu wakutupa chini
  Ee Yesu tusaidie
  Tujue kutubu hima
  Tuangukapo madhambini