Tumekosa Kweli Tumekosa

Tumekosa Kweli Tumekosa
Performed by-
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
Views4,261

Tumekosa Kweli Tumekosa Lyrics

  1. Tumekosa Kweli tumekosa
    Tunaomba Bwana Tusamehe
    Makosa yetu twayatubu

  2. Tumekukosea Bwana, tukafuata njia zetu
    Tukakuacha ee Bwana
  3. Tumekukosea Bwana, tukafuata makosa yetu
    Utusamehe Bwana
  4. Tumekukosea Bwana, twajifanya wa hekima
    Twakuzidi ee Bwana
  5. Tumekukosea Bwana, twajifanya ni miungu
    Yetu sisi wenyewe
  6. Tumekukosea Bwana, twachukua nafasi yako
    Ukawa chini yetu
  7. Tumekukosea Bwana, twajifanya twalingana
    Na wewe Mungu wetu
  8. , Tumekukosea Bwana, twajifanya tuna nguvu
    Twakushinda ee Mungu
  9. Tumekukosea Bwana, tumekosa imani kwako
    Uliye Mungu wetu
  10. Tumekukosea Bwana, tumekosa tumaini kwako,
    Ewe Muumba wetu
  11. Tumekukosea Bwana, tumekosa upendo kwako
    Na kwa jirani zetu