Kwa Nini Wanipiga

Kwa Nini Wanipiga
ChoirMoyo Mtakatifu wa Yesu Singida
AlbumUtukufu wa Bwana
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
ComposerG. Mmole
Musical Notes
Time Signature2
4
Music KeyG Major
NotesOpen PDF

Kwa Nini Wanipiga Lyrics

{ Kama nimesema vibaya toa ushahidi wa neno baya
Bali kama nimesema vema kwanini wanipiga? } *2

 1. [ s ] Pilato alimhukumu Yesu, ingawa hakuona kosa kwake
  Aliwaogopa Wayahudi, na kubembeleza urafiki wa Kaisari
 2. Ndugu yangu tafakari kwa makini, mamlaka ulopewa na wenzio
  Unayatumia ipasavyo au waumiza wenzako kama Pilato
 3. Askari usalama wa raia, acheni kuwadhulumu raia,
  Na kusingizia watu kesi, mnasababisha uvunjaji wa sheria
 4. Mahakimu na mabingwa wa sheria, haifai kuipotosha sheria,
  Maskini wajane na yatima mnawanyang`anya haki zao hukumuni
 5. Waganga wakunga na wauguzi, tibuni bila kudai zawadi,
  Watu masikini na yatima wanahangaika vitandani hadi kufa
 6. Wanandoa tunzeni ahadi zenu, kupendana katika shida na raha,
  Pia kuwalea wana katika njia impasayo Mkristo
 7. Utoaji wa mimba bila sababu, na kutupa watoto majalalani,
  Ni kutoujali utu wa mtu, na kuwahukumu kifo wasio na kosa
 8. Dunia yetu inawaka moto, amani yetu imeshatoweka,
  Vita vyatawala kila kona kisa ni tamaa ya mali na madaraka