Login | Register

Sauti za Kuimba

Misa Fadhili Lyrics

MISA FADHILI

BWANA UTUHURUMIE (MISA FADHILI)

 1. Bwana Bwana utuhurumie ee Bwana
  Bwana (Bwana) Bwana, Bwana utuhurumie
  (Ee Bwana) - Bwana, Bwana utuhurumie
 2. Kristu Kristu . . .
 3. Bwana Bwana . . .

UTUKUFU (MISA FADHILI)

Utukufu kwa Mungu Mbinguni

Utukufu (kwako) Mungu Mbinguni
Na amani (kote) duniani
Kwa watu wa mapenzi mema.

 1. Tunakuheshimu tunakusifu,
  Tunakuabudu twakutukuza ee Bwana
 2. Tunakushukuru mfalme wa mbingu
  Mwana wa pekee mwana wa Baba ee Bwana
 3. Unayeondoa makosa yetu
  Utuhurumie tusikilize ee Bwana
 4. Kuume kwa Baba unapoketi
  Mtakatifu mkuu tuhurumie ee Bwana
 5. Roho Mtakatifu pamoja nawe,
  Ndani yake Bwana unatukuzwa ee Bwana

NASADIKI KWA MUNGU (MISA FADHILI)

 1. Nasadiki kwa Mungu Baba Mwumba wa vyote
  Nasadiki kwa Yesu Kristu, Mwana wa pekee
  Nasadiki ninasadiki *2
 2. Kwa uwezo wa Roho, Mungu katwaa mwili
  Na hapo Bikira Maria kawa mamaye
 3. Kwa amri ya Ponsyo Pilato, kasulubiwa
  Akafa kazikwa akashukia kuzimu
 4. Siku ya tatu kafufuka kapaa Mbinguni
  Kaketi kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi
 5. Atarudi siku ya mwisho kutuhukumu
  Nasadiki kwa Roho Mfariji Mtakatifu
 6. Kanisa pia takatifu la Katoliki
  Ushirika wa watakatifu wa Mbinguni
 7. Na maondoleo ya dhambi kwa ubatizo
  Fufuko wa miili uzima wa milele

MTAKATIFU (MISA FADHILI)

 • Mtakatifu, mtakatifu Bwana
  Mtakatifu Mungu wa majeshi
  Mbingu na dunia zimejaa, zimejaa utukufu wako
 • Hosanna *5 Hosanna juu mbinguni *2
 • Mbarikiwa yeye ajaye kwa jina lake Bwana

FUMBO LA IMANI

 • Ee Bwana tunatangaza kifo chako
  Na kutukuza ufufuko wako
  Mpaka utakapokuja, mpaka utakapokuja

JINA LAKO BABA (MISA FADHILI)

Jina Lako Baba litukuzwe
Utawale petu milele yote *2

 1. Baba yetu mwema uliye mbinguni
  Jina lako Baba litukuzwe
 2. Na ufalme wako uje hapa kwetu
  Na mapenzi yako yatimilike
 3. Tupe leo mkate wa kila siku
  Tupe leo mkate wa kila siku
 4. Na utusamehe makosa yetu
  Kama tufanyavyo kwa ndugu zetu
 5. Situtie Baba kishawishini
  Bali maovuni utuopoe
 6. Ufalme na nguvu na utukufu
  Vyote vyako Baba hata milele

MWANAKONDOO WA MUNGU (FADHILI)

 1. Mwanakondoo wa Mungu
  Unayeondoa dhambi za dunia ee Bwana
  Tuhurumie, tuhurumie
 2. Mwanakondoo . . .
 3. Mwanakondoo wa Mungu
  Unayeondoa dhambi za dunia ee Bwana
  Tujalie amani
Misa Fadhili
CATEGORYMisa (Sung Mass)




 • Comments