Misa Kariobangi Lyrics

MISA KARIOBANGI

@ Samuel Ochieng MakOkeyo

UTUHURUMIE (MISA KARIOBANGI)

 1. [ v ] Utuhurumie
  [ w ] Ee Bwana, ee Bwana, ee Bwana
  [ v ] Tuhurumie
  [ w ] Ee Bwana, ee Bwana, ee Bwana, Bwana utuhurumie
 2. Utuhurumie
  Ee Kristu, ee Kristu, ee Kristu
  Tuhurumie
  Ee Kristu, ee Kristu, ee Kristu, Kristu utuhurumie
 3. Utuhurumie - ee Bwana . . .

  UTUKUFU JUU (MISA KARIOBANGI)

  Utukufu juu kwa Mungu,
  Utukufu juu Mbinguni
  Na amani kote duniani,
  kwa wenye mapenzi mema

  1. Tunakusifu tunakuheshimu,
   Tunakuabudu tunakutukuza
   Twakushukuru kwa ajili,
   Ya utukufu wako mkuu
  2. Ewe Mungu ndiwe mfalme,
   Wa mbinguni Baba Mwenyezi
   Ewe Bwana Yesu Kristu,
   Wa pekee mwana wa baba
  3. Ewe Yesu Mwanakondoo,
   Wa Mungu mwana wa Baba
   Ewe mwenye kuziondoa,
   Dhambi zetu tuhurumie
  4. Ewe mwenye kuziondoa,
   Za dunia dhambi za watu
   Ewe mwenye rehema nyingi,
   Upokee maombi yetu
  5. Uketiye kuume kwake,
   Mungu Baba tuhurumie
   Kwa kuwa ndiwe uliye,
   Peke yako Mtakatifu
  6. Peke yako ni wewe Bwana,
   Peke yako Bwana Mungu
   Peke yako ni Mkombozi,
   Peke yako Yesu Kristu
  7. Naye Roho Mtakatifu,
   Katika utukufu wake
   Mungu mmoja anayeishi,
   Na kutawala milele yote

   NASADIKI KWA MUNGU (MISA KARIOBANGI)

   1. Nasadiki kwa Mungu mmoja - ninasadiki
    Ndiye Baba yetu mwenyezi -
    Mwumba mbingu pia dunia -
    Nasadiki kwa Yesu Kristu -

    Nasadiki nasadiki -ninasadiki
    Nasadiki nasadiki -ninasadiki

   2. Mwana wa pekee wa Mungu -
    Mwenye kuzaliwa kwa Baba -
    Akapata mwili kwa Roho -
    Kazaliwa naye Bikira -
   3. Kisha yeye kasulubiwa -
    Kwa amri ya Ponsio Pilato -
    Kwa ajili yetu kateswa -
    Akafa na akazikwa -
   4. Kafufuka katika wafu -
    Kapaa juu Mbinguni -
    Ameketi kuume kwake -
    Mungu Baba yetu Mwenyezi -
   5. Ndipo atakapotokea -
    Kuhukumu wazima na wafu -
    Kwake Roho Mtakatifu -
    Kwa kanisa la Katoliki -
   6. Ushirika wa watakatifu -
    Ondoleo la dhambi zetu -
    Nangojea ufufuko wa miili -
    Na uzima wa milele -

   MTAKATIFU (MISA KARIOBANGI)

   • Mtakatifu
    Mtakatifu Mtakatifu Bwana Mungu
    Wa majeshi
    Mbingu na dunia zimejaa tukufu wako
   • Hosanna, Hosanna juu Mbinguni
    Hosanna, Hosanna juu Mbinguni
   • Mbarikiwa
    Anayekuja kwa jina lake Bwana Mungu

   FUMBO LA IMANI (MISA KARIOBANGI)

   • Kristu - alikufa, Kristu - alifufuka
    Kristu Yesu - alikufa, alifufuka, atakuja tena

    BABA YETU (MISA KARIOBANGI)

    Baba yetu uliye Mbinguni, Jina lako litukuzwe
    Ufalme wako ufike utakalo lifanyike

    1. Duniani kama Mbinguni -utakalo lifanyike
     Tupe leo mkate wetu -
     Mkate wetu wa kila siku -
    2. Tusamehe makosa yetu -
     Kama vile twawasamehe -
     Waliotukosea sisi -
    3. Situtie majaribuni -
     Walakini utuopoe -
     Maovuni utuopoe -
    4. Kwa kuwa ufalme ni wako -
     Na nguvu na utukufu -
     Utukufu hata milele -

     EE MWANAKONDOO (MISA KARIOBANGI)

     1. [ S ] Ee Mwanakondoo
      [ w ] Uondoaye dhambi za dunia utuhurumie } *2
     2. Ee Mwanakondo . . .
     3. Ee Mwanakondoo
      Uondoaye dhambi za dunia utujalie amani
     Misa Kariobangi
     COMPOSERSamuel Ochieng MakOkeyo
     CATEGORYMisa (Sung Mass)
     MUSIC KEYA Flat Major
     TIME SIGNATURE4
     4
     NOTES Open PDF


     Misa Kariobangi is one of the top widely sung masses in Kenya, known to almost every choir in Kenya.
     • Comments