Misa Taita

Misa Taita
Performed by-
CategoryMisa (Sung Mass)
Views10,423

Misa Taita Lyrics

BWANA UTUHURUMIE(MISA TAITA)

  1. Bwana Bwana utuhurumie
    Bwana Bwana utuhurumie
    Ee Bwana ee, ee Bwana ee!
    Ee Bwana utuhurumie
  2. Kristu Kristu utuhurumie
    Kristu Kristu utuhurumie
    Ee Kristu ee, ee Kristu ee
    Ee Kristu utuhurumie
  3. Bwana Bwana utuhurumie . . .

TUKUFU (MISA TAITA)

  1. [ v ] [ w ]
  2. Tukufu! Tukufu kwa Mungu juu
    Amani! Na amani duniani
    Kwa watu wenye mapenzi! wenye mapenzi mema *2
    A-ma-ni!
  3. Sifa! Sisi tunakusifu
    Heshima! Sisi tunakuheshimu
    Tunakuabudu! Sisi tunakuabudu *2
    He-shi-ma!
  4. Tukufu! Sisi tunakutukuza
    Shukrani! Sisi tunakushukuru
    Kwa ajili ya utukufu! Utukufu wako mkuu *2
    Shu-kra-ni!
  5. EeMungu! Ee Bwana Mungu
    Ee Baba! Mfalme wa Mbinguni
    Ee Mungu Baba! Mungu Baba Mwenyezi *2
    Ee Ba-ba!
  6. Ee Bwana! Ee Bwana Yesu Kristu
    Ee Mwana! Kristu mwana wa pekee
    Mwana wa Baba! Mwanakondoo wa Mungu *2
    Ee -Mwa-na!
  7. Mwokozi! Mwenye Kuondoa dhambi
    Huruma! Dhambi za dunia
    Utuhurumie! Pokea ombi letu *2
    Hu-ru-ma!
  8. Ee Yesu! Kwani ndiwe mtakatifu
    Ee Kristu! Kwani ndiwe Bwana
    Ewe Yesu Kristu! Ndiwe peke yako mkuu *2
    Ee Kri- stu!
  9. Umoja! Pamoja na Roho Mtakatifu
    Milele! Katika utukufu
    Tukufu wa Mungu Baba! Kristu anaishi *3
    Mi-le-le!

NASADIKI (MISA TAITA)

  1. Nasadiki kwa Mungu mmoja *2
    Mwumba mbingu na dunia *2
    Na kwa Bwana Yesu Kristu -
    Mwana wake wa pekee

    Nasadiki kwa Mungu Baba -
    Nasadiki nasadiki Mungu aliyetuumba
    Nasadiki nasadiki
    Na kwa mwana mkombozi -
    Na kwa Roho wa uzima -
  2. Alitungwa kwa uwezo wake *2
    Roho mtakatifu *2
    Kazaliwa na Maria
    Yule mama na bikira
  3. Akateswa kwa Pilato ndipo *2
    Akasulubiwa *2
    Kafa tena akazikwa
    Akashuka kuzimu
  4. Siku ya tatu kafufuka, akapaa *2
    Hata mbinguni *2
    Amekaa kuume kwa Mungu
    Baba aliye Mwenyezi
  5. Atakuja kuhukumu wazima pia *2
    Na wafu *2
    Na ufalme utakuwa
    falme wake wa milele
  6. Nasadiki kwa kanisa takatifu *2
    Takatifu Katoliki - Katoliki
    Shirika la watakatifu
    Maondoleo ya dhambi zetu
  7. Nangojea ufufuko wa miili *2
    Toka kwa wafu *2
    Na uzima wa milele
    Yote hayo nasadiki

MTAKATIFU (MISA TAITA)

  • { Mtakatifu Bwana Mungu wetu
    Ee, hosanna juu! } *3
    Mbinguni - mbinguni
  • Utukuzwe Bwana Mungu - ee
    Mungu muumba wetu - ee
    Mbingu na dunia zimejaa - ee! ee! ee!
    Utukufu wako - ee hosanna juu
    Ee ee mbinguni - mbinguni
  • Utukuzwe Bwana Mungu - ee
    Mungu mkombozi wetu - ee
    Uliangamiza mauti ukaleta - ee! ee! ee!
    Uzima mpya - ee hosanna juu
    Ee ee mbinguni - mbinguni
  • Utukuzwe Bwana Mungu -ee
    Mungu mfariji wetu - ee
    Ulimtuma roho kwetu tuwe - ee! ee! ee!
    Sote mwili mmoja - ee hosanna juu
    Ee ee mbinguni - mbinguni

FUMBO LA IMANI (MISA TAITA)

  • Kristu Kristu ee! Kristu alikufa
    Kristu Kristu ee! Kristu alifufuka
    Kristu, ee Kristu Kristu! Atakuja tena Kristu.

BABA YETU ( MISA TAITA)

  1. Baba yetu uliye mbinguni -
    Baba yetu, Baba yetu

  2. Jina lako litukuzwe daima -
    Ee Baba, ee Baba, ee!
    Baba yetu uliye mbinguni
    Jina lako litukuzwe, ufalme wako ufike
    Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni
  3. Utupe leo mkate wetu wa kila siku
    Utusamehe makosa yetu,
    Kama tunavyowasamehe
    Na sisi waliotukosea,
    Usitutie katika kishawishi
    Lakini utuopoe maovuni
  4. Kwani ufalme ni wako - Baba yetu
    Kwani nguvu ni zako - Baba yetu
    Utukufu ni wako - Baba yetu
    Baba milele milele -Hizi zote zako Baba!
  1. MWANAKONDOO (MISA TAITA)

  2. Mwana - Mwanakondoo wa Mungu
    Uondoaye - uondoaye
    Dhambi za dunia - dhambi za dunia
    Utuhurumie - utuhurumie
  3. Mwana - Mwanakondoo wa Mungu
    Uondoaye - uondoaye
    Dhambi za dunia - dhambi za dunia
    Utuhurumie - utuhurumie
  4. Mwana - Mwanakondoo wa Mungu
    Uondoaye - uondoaye
    Dhambi za dunia - dhambi za dunia
    Utujalie - amani