Login | Register

Sauti za Kuimba

Misa Paulo Lyrics

MISA PAULO

@ Emmanuel Kilonda

BWANA UTUHURUMIE (MT. PAULO)

 1. Wewe uliyetumwa kuwaponya wanaojuta dhambi
  Ee Bwana utuhurumie, ee Bwana utuhurumie
  Bwana, Bwana, ee Bwana, ee Bwana utuhurumie
 2. Wewe uliyekuja kuwaita wakosefu
  Ee Kristu, utuhurumie, ee Kristu, utuhurumie
  Kristu, Kristu, ee Kristu, ee Kristu, utuhurumie
 3. Wewe unayeketi kuume kwa Baba, ukituombea,
  Ee Bwana utuhurumie, ee Bwana utuhurumie
  Bwana, Bwana, ee Bwana, ee Bwana utuhurumie

  UTUKUFU (MISA PAULO)

  Utukufu (utukufu), utukufu (utukufu),
  Utukufu kwa Mungu juu mbinguni
  Na amani (na amani) duniani (duniani)
  Kwa watu wenye mapenzi mema

  1. Tunakusifu Bwana, tunakuheshimu,
   Tunakuabudu (Bwana), tunakutukuza,
   Tunakushukuru (tunakushukuru)
   Kwa ajili ya utukufu wako mkuu *4
  2. Ee Bwana Mungu, Mfalme wa Mbinguni,
   Ee ee Bwana Mungu, Mungu Baba Mwenyezi.
   Ee Bwana Yesu Kristu, Mwana wa pekee *2
   Ee Bwana Mungu, (ee Bwana Mungu)
   Mwanakondoo wa Mungu mwana wa Baba *4
  3. Mwenye kuondoa dhambi za dunia,
   Utuhurumie, pokea ombi letu
   Ee Mwenye kuketi (ee mwenye kuketi)
   Kuume kwa Baba tuhurumie *4
  4. Kwa kuwa ndiwe, peke yako Mtakatifu,
   Peke yako Bwana Mkuu, peke yako Yesu Kristu
   Pamoja na roho (Roho Mtakatifu)
   Katika utukufu wa Mungu Baba *4

   NASADIKI (MT. PAULO)

   Nasadiki - nasadiki, nasadiki - nasadiki *2

   1. Nasadiki kwa Mungu Baba Mwenyezi
    Muumba wa Mbingu na dunia
    Na Yesu Kristu Mwanaye wa pekee,
    Mungu kweli na mtu kweli
   2. Aliyepata mwili kwa uwezo,
    Wa Roho Mtakatifu
    Kwake yeye Bikira Maria,
    Akawa mwanadamu
   3. Akasulubiwa, akateswa,
    Kwa mamlaka ya Ponsyo Pilatu
    Na akafa, akazikwa,
    Akashuka kuzimuni mmh mmh mmh
   4. Akafufuka siku ya tatu
    Akapaa Mbinguni aah aah
    Amekaa kuume kwake Baba
    Atakuja tena kuwahukumu, wazima na wafu
   5. Nasadiki kwa Roho Mtakatifu,
    Kanisa Takatifu Katoliklugha i
    Maondoleo ya dhambi, ufufuko wa wafu,
    Uzima wa milele Amina

   MTAKATIFU (MT. PAULO)

   • { Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu
    Bwana Mungu wa majeshi } *2
   • { Mbingu na dunia zimejaa,
    Utukufu wako Bwana } *2
   • { Hosanna juu, Hosanna juu
    Hosanna juu, Hosanna juu Mbinguni } *2
   • { Mbarikiwa anayekuja, kwa jina la Bwana } *2

    MWANAKONDOO (MT. PAULO)

    1. Mwanakondoo, ee Mwanakondoo
     Ee Mwanakondoo wa Mungu
     Uondoaye dhambi za dunia,
     { Utuhurumie, utuhurumie } *2 huruma!
    2. Mwanakondoo, ee Mwanakondoo
     Ee Mwanakondoo wa Mungu
     Uondoaye dhambi za dunia,
     { Utuhurumie, utuhurumie } *2 huruma!
    3. Mwanakondoo, ee Mwanakondoo
     Ee Mwanakondoo wa Mungu
     Uondoaye dhambi za dunia,
     { Utujalie amani } *2 amani
    Misa Paulo
    COMPOSEREmmanuel Kilonda
    CATEGORYMisa (Sung Mass)
    • Comments